Sanaa za Kipekee
zisizo na mpinzani
ZILIZOCHAGULIWA KUTOKA KATIKA MKUSANYIKO WA MAKUMBUSHO
MAONESHO YA MUDA
" Fiziognomia za tofauti za sanaa za kiafrika zinastaajabisha. Ndio maana kuna sanaa chache sana duniani zinazoweza kushindanishwa nazo hasa kwa wingi wake. Kwa ubunifu wake wa kushangaza, utajiri na wingi wa muunganiko wa maumbo na mistari (…) aina hii ya sanaa haina mpinzani duniani."
Vladimir Markov, (Sanaa ya Watu Weusi), 1919
Makabrasha manne yaliyopo katika chumba hiki, yanaonesha mkusanyiko wa barakoa, sanamu, michongo ya pembe za ndovu na matumizi ya sanaa. Karibia kila ukionacho, kinatoka Kongo na vimefika hapa mnamo karne ya 19 na nusu ya kwanza ya karne ya 20.
Maonesho mengine yanaonesha mambo mahususi kama vile dhana ya urembo katika Afrika, mtazamo wa Ulaya katika sanaa za Kiafrika, utambulisho wa wasanii au uchambuzi wa kimitindo.